Baada ya Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule ‘Prof Jay’ kusimama bungeni na kumtetea Diamond kuhusu kudaiwa na TRA, mwanamuziki huyo ametumia ukurasa wake wa Instagram kumsifia mbunge huyo.

Kupitia ukurasa wake huo wa Instagram Diamond ameweka video ya mbunge huyo akiongea bungeni kuhusu suala la kumtetea kuhusu kudaiwa na mamlaka ya mapato Tanzanai (TRA).

Kwenye hotuba yake Bungeni Profesa Jay amesema kuwa “Juzi Msanii Diamond alikua analalamika TRA wamempelekea kodi ya Milioni 400, unaweza kujiuliza anadaiwa milioni 400 kwa kiasi gani alichoingiza?‘.

Pia mProfesa Jay amesema kuwa “Downloads zinazofanyika mnaweza kuona Wasanii sasa hivi wanabanwa, TRA wanatamani kuvuna kutoka kwa Wasanii kitu ambacho bado hawajakipandikiza.

Amendelea kusema kuwa ‘tumekua na ule msemo kama wa zamani kwamba shamba likiwa na bangi ni lako lakini likiwa na dhahabu ni la serikali… tunataka kuchuma kitu ambacho hatujakipanda, inabidi Serikali ianze kuwekeza na kuwajenga Wasanii kutoka shule za msingi mpaka Chuo kikuu”

Baada ya maneno hayo ya Profesa Jay kwenye video, Diamond Platnumz aliichukua video hiyo na kuandika; “Ndio Maana kwenye Jimbo lako sikuja kupiga kampeni bro…kwakuwa niliijua mapema thamani na umuhimu wa Uwepo wako kwenye hilo jengo”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *