Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz A.K.A Simba ametumia akaunti yake ya Tittwer kumshukuru mpenzi wake Zari kwa mchango mkubwa aliofanya kwenye maisha yake mpaka kufanikiwa.

Diamond amesema kuwa Zari amebadilisha sana maisha yake baada ya kumzalia mtoto wake wa kwanza Tiffa ambapo kitendo hiko kimesababisha afocus sana kwenye kazi yake kutokana na kuwa baba.

Mwanamuziki huyo kupitia akaunti yake hiyo ameandika “Zari Mchango wake ni mkubwa sana kwenye maisha yangu aliponizalia mtoto ilinipa focus ya maisha na pia hunipa ushauri mwingi sana wa maisha”.

Diamond Platnumz ni mwanamuziki mwenye mafanikio makubwa sana hapa nchini kutona na kazi yake ya muziki ambapo anamiliki nyumba hapa nchini pamoja na Afrika Kusini na vitu vingine vya thamani.

Wiki iliyopita Diamond amezindua mtandao wake wa kuuza nyimbo kwa wasanii nchini unaojulikana kwa jina la ‘Wasafi.com.

Zari na Diamond wamefanikiwa kupata watoto wawili ambao ni Tiffa na Prince Nillan aliyezaliwa nchini Afrika Kusini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *