Mtayarishaji wa muziki kutoka katika studio za AM Records, Manecky amefunguka na kusema kuwa yeye anapenda sana kufanya kazi na wasanii chipukizi.

Amesema kupitia wasanii hao yeye kama producer anaweza kuonesha uwezo wake katika kufanya muziki tofauti na kufanya kazi na wasanii ambao tayari ni wakubwa au ambao wapo kwenye soko kwa wakati huo.

Manecky amedai kuwa yeye kama mtayarishaji anaweza kuonesha uwezo wake pindi anapofanya kazi na wasanii wachanga na wasanii ambao wamepotea kwenye game tofauti na wasanii wenye majina kwa sasa.

Manecky amesema kuwa “Mimi huwa napenda kufanya kazi na ‘undergrounds’ kwa sababu kupitia hao wasanii naweza kuonesha uwezo wangu kama producer hawa wasanii wakubwa wanaweza kukubana kuonesha uwezo wako, lakini leo hii ukifanya na mwanamuziki mkubwa ni kweli utafahamika na utakuwa unasikika mara kwa mara lakini siku akiacha kufanya kazi na wewe ndiyo na wewe umeshapotea kwenye ramani, lakini ukiweza kumtoa msanii mchanga na kuwa mkubwa ina maana utakuwa na uwezo wa kumtoa mwingine na kuwa mkubwa pia, hivyo utaendelea kuwepo kwenye tasnia siku zote”.

Manecky ni mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini ambaye amewahi kushinda tuzo ya producer bora kutokana na kazi zake alizaowahi kufanya hapo nyuma.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *