Mshambuliaji wa Liverpool, Sadio Mane ameshinda tuzo ya mchezaji wa bora wa klabu ya Liverpool msimu wa 2016/17.

Mane alitangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa klabu hiyo baada ya kumshinda Philippe Coutinho.

Mane ameshinda tuzo hizo baada ya kuwa katika kiwango bora tangu alipotua Liverpool mwezi Agosti mwaka jana akitokea Southampton kwa ada ya Pauni Milioni 32.

Mane ndiye mfungaji bora Liverpool akiwa amefunga mabao 13 kwenye michuano tofauti nchini Uingereza.

Wengine waliochomoka na tuzo ni Trent Alexander-Arnold,18, aliyeshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi.

Ben Woodburn ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa kituo cha kulea na kukuza vipaji kwa vijana cha Liverpool (Academy).

Emre Can ametwaa tuzo ya bao bora la mwaka, baada ya bao lake la tiki taka alilofunga dhidi ya Watford  kuonekana kuwa bora zaidi kuliko mabao yote yaliyofungwa na Liverpool msimu wa 2016/17.

Lucas Leiva amepewa tuzo ya heshima baada ya kufikisha miaka kumi (10) akiwa klabuni Liverpool.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *