Manchester United wamefanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora kwenye ligi ya Europa baada ya kushinda 1-0 dhidi ya Saint-Etienne.

Goli la Mnchester United limefungwa na Henrikh Mkhitaryan ambaye aliumia na kulazimika kuondoka uwanjani wakati wa mechi hiyo.

Muda mfupi baadaye hata hivyo, mchezaji huyo kutoka Armenia alionekana kuumia misuli ya paja na kulazimika kuondoka wuwanjani.

Manchester United walikuwa mbele 3-0 kutokana na ushindi wa mechi ya mzunguko wa kwanza ambapo magoli yote yakifungwa na Zlatan Ibrahimovic.

Beki wao Eric Bailly pia alitolewa nje dakika ya 63 baada ya kuonesha kadi ya pili ya njano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *