Klabu ya Manchester United imeshinda 5-2 dhidi ya Los Angeles Galax kwenye mechi ya kirafiki iliyofanyika usiku wa kuamkia leo nchini Marekani.

Katika mechi hiyo kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ameanzisha kikosi kingine na kipindi cha pili kuanzisha kikosi kingine.

Magoli ya Manchester United yamefungwa na mshmbuliaji wake, Marcus Rashford aliyefunga goli la kwanza na la pili huku goli la tatu likifungwa na Fellaini.

Goli la nne limefungwa na kiungo, Henrick Mikkhitaryan baada ya kupokea pasi kutoka kwa Anthony Martial.

Goli la tano limefungwa na Anthony Martial baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa beki Fosu-Mensah.

Mechi hiyo ni ya kwanza kwa Manchester United ambayo ipo Marekani kujiandaa na msimu ujao wa ligi kuu nchini Uingereza.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *