Manchester United imefungwa  1-0 dhidi ya Feyenoord kwenye mechi ya kundi A kombe la Europa ligi iliyoafanyika katika uwanja wa Stadion Feijenoord nchini Uholanzi jana usiku.

Kabla ya dakika 90 za mchezo huo kumalizika kwa Man United kuondoka vichwa chini kwa kukubali kipigo cha goli 1-0 lililofungwa na Tonny Vilhena dakika ya 79, takwimu ilikuwa inaonesha mara ya mwisho Novemba 5 1997 Man United alicheza katika uwanja huo na kuondoka na ushindi wa goli 3-1.

rashford

Rekodi dhidi ya Feyenoord haikuisaidia Man United na badala yake wameondoka na huzuni kwa kuvunjwa rekodi yao ya kufungwa mechi nne za Europa League mfululizo ugenini katika historia , Man United sasa watashuka dimbani Septemba 29 Old Trafford kucheza dhidi ya Zorya ya Ukraine katika mchezo wao wa pili.

pogba

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *