Klabu ya Manchester United imekubali kumuuza kiungo wake, Morgan Schneiderlin kwenda Everton kwa ada ya uhamisho itakayogharimu paundi milioni 22.

Kiungo huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 27 alijiunga na Manchester United akitokea Southampton ambapo alisajiriwa na aliyekuwa kocha wa wakati huo Louis Van Gaal kwa ada ya uhamisho paundi milioni 25 Julai 2015.

Mchezaji huyo amecheza mechi 47 toka ajiunge na Manchester United ukijumlisha na mechi nane chini ya kocha Jose Mourinho huku akicheza mechi za ligi kuu tatu tu.

Baada ya mechi ya jana dhidi ya Hull City ambapo Manchester United ilishinda 2-0, Kocha wa timu hiyo Jose Mourinho amesemakuwa Makamo Mwenyekiti, Ed Woodward amemfahamisha kila kitu kipo sawa na Morgan anajiunga na Everton.

Pia Schneiderlin alikuwa anawindwa na klabu ya West Brom lakini ameamua kujinga kwa mara ya pili na aliyekuwa kocha wake  wakati akiwa Southampthon, Ronald Koeman.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *