Manchester United wakubali kumuuza Depay kwenda Lyon

0
248

Klabu ya Manchester United imekubali kumuuza winga wao Memphis Depay kwenda klabu ya Lyon kwa ada paundi milioni 16 huku dau likipanda hadi kufikia paundi milioni 21 kma Lyon watafuzu klabu bingwa Ulaya.

Mshambuliaji huyo wa Uholanzi mwenye miaka 22 ameshinda goli saba katika mechi 53 toka ajiunge Manchester United kwa ada ya uhamisho paundi milioni 31 akitokea PSV mwaka Mei 2015.

Lyon inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu Ufaransa ikiachwa alama 11 na anayeongoza ligi hiyo kiongozi wa ligi hiyo Monaco.

Depay amecheza mechi nane msimu huu chini ya kocha Jose Mourinho ambaye ajahamasishwa na kiwango cha mshambuliaji huyo kutoka Uholanzi.

 

LEAVE A REPLY