Klabu ya Manchester United watakutana na beki wake wa zamani Jaap Stam baada ya Reading kupangwa na United kwenye hatua ya 32 bora michuano ya Kombe la FA.

Kocha wa Reading ni beki wa zamani wa Manchester United Jaap Stam ambaye alifundisha na kocha alitundika daruga Sir Alex Ferguson.

Kwa upande wa Chelsea wao watakutana na mshindi kati ya Petersborough na Notts County kwenye hatua hiyo ya 32 bora ya kombe la FA.

Michuano hiyo ya raundi ya tatu itachezwa kati ya 6 na 9 Januari mwakani.

West Ham watakuwa wenyeji wa Manchester City kwenye mechi itakayokutanisha klabu za Ligi za kuu huku Everton wakiwa wenyeji wa Leicester City.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *