Manchester United itakutana na Ajax kwenye fainali ya Europa ligi itakayofanyika katika Uwanja wa Friends Arena katika mji wa Stockholm nchini Sweden ifikapo Mei 24 mwaka huu.

Manchester United na Ajax zimefuzu kwenye fainali  hiyo baada ya kuchomoza na matokeo  mazuri kwenye zao za jana licha ya Man U kutoka 1-1 na Ajax kufungwa 3-1.

United ambao walikuwa kwenye Uwanja  wa Old Traff  kuvaana na Celta Vigo  walifanikiwa kuchomoza na sare ya bao  1-1, lakini wakafuzu kwa fainali baada ya  kushinda 1-0 kwenye mchezo wa kwanza  nchini Hispania wiki moja iliyopita.

Huu ulikuwa ushindi muhimu kwa kocha wa United Jose Mourinho, ambaye alishasema kuwa anachotazama sasa ni kutwaa ubingwa huo ili aweze kupata nafasi ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Katika dakika ya 17 ya mchezo  Celta Vigo walipata wakati mgumu baada ya kiungo wa United, Marouane Fellaini kuifungia timu yake bao baada ya kumalizia pasi iliyopigwa na Marcus Rashford.

Katika dakika ya 85 baada ya Roncaglia kuwasazishia bao hilo na kuwapa presha kubwa United.

Mpaka filimbi ya mwisho ya mchezo huo matokeo yalikuwa 1-1 kwa timu hizo ambapo matokeao hayo yalikuwa na faida kwa Manchester United baada ya kushinda katika mechi ya kwanza iliyofanyika Uhispania.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *