Manchester United leo itawakosa wachezaji wake watano kwenye mechi dhidi ya West Brom itakayofanyika katika uwanja wa Old Trafford kutokana na sababu tofauti.

Mabeki Chris Smalling na Phil Jones ambao walipata majeraha ya kuwaweka nje kwa muda mrefu walipokuwa wanachezea timu ya taifa ya Uingereza.

Kutokana na kuumia kwa Smalling na Jones, Mourinho amemwita beki wa miaka 19 Axel Tuanzebe kikosini kwa ajili ya mechi hiyo.

Pia Manchester United wataendela kuwakosa mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic na kiungo wa kati Ander Herrera wanao tumikia adhabu.

Mwingine Paul Pogba anayeuguza jeraha la misuli ya paja aliyoyapata kwenye mechi ya nyumba.

Kwa upande mwingine nahodha wa United Wayne Rooney atarejea kucheza dhidi ya West Brom Jumamosi baada ya kupona jeraha la goti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *