Kiungo wa Manchester United, Henrikh Mkhitaryan atakosa mechi mbili za ligi kuu nchini Uingereza baada ya kuumia kifundo cha mguu wakati wa ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Tottenham jana.

Mkhitaryan amechezewa visivyo na beki wa kulia wa Spurs Danny Rose na baada ya kupata matibabu muda mrefu uwanjani aliondolewa kwenye machela dakika ya 85.

Kwa upande wake kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amesema jeraha hilo si baya sana kwa mchezaji huyo.

Pia Mourinho awali aliuwa na wasiwasi kwamba jeraha hilo lingekuwa mbaya lakini baadaye akasema watamkosa kwa wiki kadha tu.

Kiungo huyo atakosa mechi ya Jumatano ugenini dhidi ya Crystal Palace na mechi ya Jumamosi dhidi ya West Bromwich Albion na anatarajiwa kurejea kucheza dhidi ya Sunderland Disemab 26.

Mkhitaryan ndiye aliyewafungia United bao hilo la ushindi dhidi ya Tottenham uwanjani Old Trafford.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *