Klabu ya Manchester United imeenda nchini China kwa ajiri ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu nchini Uingereza itakayoanza mwezi Agosti mwaka huu.

Klabu hiyo itacheza mechi mbili za kirafiki kabla ya kurejea ambapo mechi ya kwanza watacheza dhidi ya Borussia Dortmund itakayofayika mjini Shanghai, siku ya ijumaa na mechi ya pili watacheza dhidi ya wapinzani wao timu ya Manchester City,jijini Beijing, siku ya jumatatu.

Jumla ya wachezaji 25 wamejumuishwa kwenye msafara wa timu hiyo wakiwamo wachezaji wao wapya Eric Bailly na Henrikh Mkhitaryan pamoja na Chipukizi tisa toka chuo cha soka cha Manchester United.

Manchester United wamekwenda katika ziara hiyo wakiwa chini ya kocha wao mpya, Jose Mourhino amabaye amechukua nafasi hiyo kutoka kwa mtangulizi wake Louis Van Gaal aliyetimuliwa mwisho wa msimu ulioisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *