Ligi kuu Uingereza leo inaendelea tena kwa mechi nane katika viwanja tofauti baada ya kupumzika kwa wiki moja kupisha mechi za kimataifa za kalenda ya FIFA kufuzu kombe la dunia.

Macho na masikio ya watu yatakuwa katika uwanja wa Old Trafford ambapo Manchester United wataikaribisha Arsenal kwenye dimba hilo kwa mara ya kwanza toka Mourinho awe kocha wa United.

Mechi hiyo itakuwa na ushindani mkubwa kuanzia ndani ya uwanja hadi nje ya uwanja kutokana na upinzani uliopo katika ya kocha wa Manchester United, Jose Mourinho na kocha wa Arsenal, Arsene Wenger.

Katika Mechi hiyo historia inambeba Manchester United kutokana na mechi kumi zilizofayika uwanja wa Old Trafford za ligi kuu nchini Uingereza Manchester United imeshinda mechi saba, sare mbili na Arsenal kushinda mechi moja.

Mechi ya mwisho ya ligi kuu kwa Arsenal kuifunga Manchester United katika uwanja wa Old Trafford ilikuwa mwaka 2006 ambapo Arsenal ilishinda 1-0 goli likifungwa na Emmanuel Adebayo akipokea pasi nzuri kutoka kwa Cess Fabregas.

Katika mechi mbili za ligi kuu walizokutana msimu wa mwaka jana kila timu moja ilishinda mechi moja moja, Arsenal ilishinda 3-0 katika uwanja wa Emarates katika mechi ya kwanza na mechi ya pili Manchester United ilishinda 3-2 katika uwanja wa Old Trafford.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *