Klabu ya Manchester City imeondolewa katika michuano ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya kufungwa 3-1 dhidi ya Monaco na kufanya matokeo ya jumla kuwa 6-6.

Kutokana na matokeo hayo Manchester City imetolewa kwenye michuano hiyo kwa sheria ya magoli ya ugenini.

Goli la kwanza la Monaco kwenye mchezo huo limefungwa na Mbappe katika dakika ya saba baada ya kuunganisha krosi ya Silva, goli la pili limefungwa na Fabinho huku goli la mwisho likifungwa na Bakayo kwa upande wa Manchester City goli limefungwa na Leroy Sane dakika ya 72.

Katika mchezo mwingine Atletico Madrid wameingia robo fainali baada ya mchezo wao dhidi ya Bayer Leverkusen kumalizika kwa sare ya 0-0 lakini mchezo wa kwanza Atletico Madrid alishinda 2-0 kwenye mchezo wa kwanza.

Droo ya robo fainali inatarajiwa kupangwa kesho siku ya Ijumaa baada ya hatua ya 16 bora kukamilika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *