Manchestester City leo imepoteza mechi ya kwanza katika ligi kuu nchini Uingereza msimu huu baada ya kupokea kichapo cha magoli 2-0 kutoka kwa Tottenham kwenye mechi iliyofanyika katika uwanja wa White Hart Lane.

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Tottenham walikuwa mbele kwa goli hizo mbili baada ya kutawala mchezo huo huku City wakionekana kukamatwa sana na kupelekea kupokea kichapo hiko.

Tottenham walipata goli lao la kwanza baada ya beki wa Manchester City, Kolarov kujifunga mnao dakika ya 9 ya mchezo huo huku goli la pili likifungwa na Dele Alli katika dakika ya 37.

Licha ya kupoteza mchezo huo bado Manchester City wanaongoza msimamo wa ligi hiyo ambapo wamejikusanyia points 18 baada ya kucheza mechi saba, akishinda sita na kufungwa moja ya leo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *