Klabu ya Manchester City imeruhusiwa kumnunua winga wa Brazil wa umri wa miaka 19 Gabriel Jesus na sasa anaweza akacheza dhidi ya Tottenham Jumamosi.

Jesus amehamia Manchester City akitokea klabu ya Palmeiras ya Brazil kwa £27m.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil alikubali kuhamia kwenye klabu hiyo kwa mkataba wa miaka mitano Agosti mwaka jana.

Jesus alifika City mwanzoni mwa mwezi huu lakini alichelewa kupata idhini ya kusajiliwa City, taarifa zikisema Shirikisho la Soka la Uingereza lilikuwa linachunguza stakabadhi kuhusu uhamisho wake.

City wanamchukulia mchezaji huyo kuwa chipukizi mwenye kipaji zaidi Amerika Kusini kwa sasa, na waliwapiku Barcelona kumchukua.

Jesus amesema meneja wa City Pep Guardiola alichangia sana katika uamuzi wake wa kuhamia klabu hiyo.

Manchester City kwa sasa wanashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza wakiwa nyuma 10 dhidi ya Chelsea wanaoshika nafasi ya kwanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *