Manchester City imepanda mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza baada ya kuifunga Bournemouth mabao 2-0.

Goli la kwanza la Manchester City limefungwa na kiungo wake Raheem Stearling katika dakika 29 ya mchezo huo.

Goli la pili la Manchester City lilikuwa la kujifunga kupitia mchezaji Tyrone Mings katika dakika ya 69 na kufanya matokeo kumalizika 2-0.

Manchester City  imefikisha pointi 52, nyuma ya Chelsea wanaoongoza ligi wakiwa na pointi 60 ambao ndiyo wanaongoza ligi hiyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *