Klabu ya Manchester City imefungwa goli 1-0 dhidi ya Bayern Munich kwenye mechi ya kirafiki iliyofanyika katika uwanja wa Allianz Arena nchini Ujerumani.

Bayern Munich kwa sasa inanolewa na kocha Carlo Ancelotti ilipata goli lake kupitia kwa  mchezaji Erdal Ozturk ambalo lilidumu hadi mwisho wa mchezo huo.

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola alitumia zaidi wachezaji vijana kwenye mechi hiyo kutokana na nyota wake wengi kuwa mapumzikoni baada ya kushiriki michuano ya Euro na Copa America mwaka huu.

Wachezaji wa Manchester City Sergio Aguero, David Silva, Nolito, Raheem Sterling na Joe Hart wataunganga na timu hiyo kwenye safari ya China kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu nchi Uingereza ambapo watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Machester United siku ya jumatatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *