Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara amerusha dongo kwa wapinzani wao wa jadi Yanga baada ya kuwaambia wanapambana na hali zao.

Manara amesema hayo kupitia akaunti yake ya Instagram baada ya kuwapongeza wachezaji wa klabu yao Simba kwa ushindi dhidi ya Stand United na kuongoza ligi Tanzania Bara.

Manara ameandika  “Sasa hivi tunaongoza ligi kwa wastani mzuri wa mabao ambayo pengine ukihesabu timu tano au nne zinazotufuata ukijumlisha mabao yao ndiyo unapata mabao yetu.

Pia ameeendelea kuandika “Kwa hiyo lazima tuwapongeze wachezaji wetu kwa kazi kubwa waliofanya, nadhani unaona wenzetu wanavyopambana na hali zao,” alisema Haji Manara.

Kwa upande mwingine, Manara pia ametoa tahadhari kwa Bodi ya Ligi na TFF kuhusu maamuzi yanayotolewa na baadhi ya waamuzi huku akimlalamikia mwamuzi kukataa bao la Laudit Mavugo kwamba mshambuliaji huyo alifunga bao akiwa katika nafasi ya kuotea.

Licha ya kuwa hajataja timu nyingine zaidi ya Simba katika maelezo yake lakini ni wazi dongo hilo linaenda kwa Yanga ambao ndiyo wapinzani wakubwa wa Simba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *