Msemaji wa klabu Simba SC, Haji Manara amesema kuwa Simba ndiyo bingwa halali wa ligi kuu Tanzania Bara msimu huu.

 Manara amesema kuwa klabu yake ndio bingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara kwa msimu wa 2016/17 na kuwataka Yanga wajipange kurudisha ubingwa huo.

Manara amesema hayo kupitia akaunti yake ya mtandao wa Instagram baada ya rufaa yao kuanza kusikilizwa na shirikisho la soka duniani (FIFA).

Kupitia akaunti hiyo Manara ameandika, ‘wabongo bana kwa ‘double standard’ hawajambo, Serengeti Boys walikuwa Gabon kwa kushinda rufaa ila Simba hawastahili. Mjiandae kiakili Gongowazi, Simba ndiyo ‘champion’ msimu huu”.

Yanga Jumamosi walikabidhiwa kombe la ubingwa msimu wa 2016/17 baada ya kutwaa ubingwa huo kutokana na tofauti ya magoli na klabu ya Simba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *