Klabu ya Manchester United imeweka tena historia nyingine kwenye soka la Uingereza baada ya kupitisha azimio la upanuzi wa eneo la kukaliwa na mashabiki walemavu ambapo zitaongezwa siti 300.

Ili kufanikisha upanuzi huo wa sehemu za kukaa mashabiki walemavu, klabu ya Manchester imelazimika kuhamisha tiketi 2,600 za msimu.

Upanuzi huo unaokadiriwa kuchukua miaka mitatu kukamilika utakamilika wakati wa kuanza kwa msimu wa 2017-18.

Tayari United wamethibitisha kuwa mashabiki 800 wenye tiketi za msimu watahamishwa kwenye eneo kutakapofanyika ujenzi huo katika msimu ujao na mashabiki wengine 1,600 watahamishwa kwenye vipindi viwili vya misimu miwili itakayofuatia.

Katibu wa chama cha Mashabiki Walemavu wa Manchester United, ‘Manchester United Disabled Supporters’ Association (MUDSA), Chas Banks amekaririwa akipongeza hatua hiyo kwa kusema:

‘Nimejawa na furaha kubwa na ninajivunia kuwa klabu ninayoipenda tangu nilipokuja Old Trafford kwa mara ya kwanza mwaka 1957 inaonyesha njia ya kuboresha maeneo ya kukaa walemavu kuendana na muongozo uliowekwa na Accessible Stadia. Ni ndoto iliyotimia kwangu na mashabiki wengine walemavu’.

screen-shot-2017-01-24-at-16-59-57

screen-shot-2017-01-24-at-16-59-39

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *