Manchester United inatarajiwa kushuka dimbani dhidi ya Southampton kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza itakayofanyika katika uwanja wa Old Trafford leo usiku.

 

paul-pogba-manchester-united_3763379

Mechi hiyo ni pili kwa timu hiyo baada ya mechi ya kwanza kushinda 3-1 dhidi ya Bournamouth iliyofanyika jumapili iliyopita na manchester United kuibuka na ushindi huo.

 

Katika mechi hiyo kiungo mpya wa Manchester United,Paul Pogba anatarajiwa kuanza baada ya kuukosa mchezo uliopita kutokana na kuwa na kadi mbili za njano alizozipata katika ligi ya Italia ambapo sheria za chama cha soka Uingereza FA huzitambua kadi hizo.

 

paul-pogba-training-manchester_3763381

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *