Leo mechi za kombe la Carabao zinaendelea nchini Uingereza kwa michezo mitano baada ya jana kushuhudia Liverpool akiyaaga mashindano hayo.

Arsenal watakuwa nyumbani Emirates wakiwakaribisha Doncaster Rovers kwenye mchezo utakaofanyika mida ya saa tatu na dakika 45 usiku.

Nottingham Fores watasafiri hadi darajani kuwafuata mabingwa wa Uingereza Chelsea kwenye mechi ya kombe hilo katika uwanja wa Stamford Bridge.

Nao Everton leo watakuwa nyumbani kuwakaribisha Sunderland kwenye mechi ya kombe hilo itakayofanyika kuanzia saa tatu na dakika 45 usiku katika uwanja wa Goodson Park.

Manchester United watakuwa nyumbani katika uwanja wa Old Trafford wakiwakaribisha Burton Albion mechi itakayoanza mida ya saa nne kamili usiku.

West Bromwich watawakaribisha vijana wa Pepe Gurdiola Manchester City kwenye mechi inayotarajiwa kuanza mida ya saa nne kamili usiku.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *