Muimbaji wa muziki wa Singeli nchini, Man Fongo amesema kuwa amepata mafanikio makubwa kwenye kupitia muziki wa Singeli kwa muda mfupi kuliko matarajiao yake ya hapo awali.

Man Fongo amesema anashangaa mafanikio makubwa ambayo ameyapata ndani ya muda mfupi kupitia muziki wa Singeli hususani kupitia kazi yake ya ‘Hainaga ushemeji’ ambayo imemtambulisha vyema kwa jamii.

Staa huyo wa Singeli amesema kuwa muziki huo umebadilisha maisha yake ndani ya muda mfupi na sasa anaona maisha kwake ni kama mepesi akilinganisha na kipindi cha nyuma.

Vile vile Man Fongo amesema muziki wa Singeli umesababisha mpaka amepanga nyumba nzima Tabata huku akimiliki gari aina ya Toyota Altezza huku akisistiza hayo ni mafanikio makubwa kwake.

Pia ameongeza kusema kwamba hayo ni mafanikio makubwa kwake yaliyokuja kwa muda mfupi sana kutoka kuishi gheto chumba kimoja mpaka sasa anaishi nyumba nzima huku familia ikimtegemea yeye.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *