Kila binadamu anapenda kufanya jambo fulani kabla ya kuanza kwa kazi yake, wengine upenda kuswali kwa kumuomba Mungu awafanyie wepesi kwenye kazi zake za kila siku.

Kwa upande wa mshambuliaji wa PSG na timu ya Taifa ya Brazil, Neymar Jr yeye amefunguka mambo matano anayofanya kabla ya kuanza kwa mechi yoyote dhidi ya wapinzani wake.

Mambo hayo matano aliyosema Neymar anayofanya kabla ya kuanza kwa mechi ni kama ifuatavyo.

1) Kuongea na Baba Yake Mzazi

Neymar ana mahusiano mazuri na baba yake,Baba yake ana nafasi kubwa kwenye maswala ya pesa ya Neymar, baba yake huchukua nafasi ya Agent wake kwenye dili tofauti kama dili ya kuhamia PSG akitokea Barcelona.

2) Anasikiliza Muziki

Wanamichezo wengi husikiliza muziki kabla ya kufanya mashindano yao, Neymar hufanya hivyo kabla ya game zake zote.

3) Hufanya Maombi.

Neymar hufanya maombi mafupi kabla ya kila mchezo na hata akifunga hushangilia kwa kunyoosha vidole juu kama ishara ya kumshukuru Mungu.

4) Huenda Msalani

Neymar anahakikisha yuko tayari kwa Game muda unapofika, lazima amalize haja zake kabla hajaingia uwanjani.

5) Kupiga picha Moja

Ili kuwa karibu na mashabiki, Neymar anapiga picha moja kabla ya game zake ilikuhakikisha followers wao kwenye mitandao kama Twitter ,Facebook na Instagram wanajua kinachoendelea.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *