Mwanamuziki wa hip hop, Roma amefunguka kuhusu tukio la utekaji lililomkuta yeye pamoja na wenzake watatu wakiwa studio za Tongwe Records zilizopo Masaki jijini Dar es Salaam.

Roma amesema kuwa walikuja watu waliokuwa na silaha za moto, wakawaamuru kuingia kwenye gari na kisha wakafungwa vitambaa usoni na pingu mkononi na kupelekwa eneo ambalo halijulikani.

Wakiwa katika eneo hilo walihojiwa kwa siku tatu huku wakipigwa kabla ya kwenda kutupwa wakiwa wamefungwa katika eneo ambalo kwa haraka hawakujua ni wapi.

Mazungumzo yake yalikuwa kama ifuatavyo

 1. Kwanza natoa shukrani kwa Mungu, kwenu, kwa wananchi na hasa wasanii wenzangu, nimeona mmesimama imara, pia serikali.

  2.Kilichotokea ni kama case study maana kimetuunganisha wote bila kujali itikadi zetu, tuendelee kushikamana.

  3.Niwaambie ukweli tu, mpaka sasa hatuna uhakika na usalama wetu, mahali tulipokuwa si pazuri kabisa.

  4.Kama alifanyiwa daktari, baadaye akafanyiwa msanii, usishtuke kesho akafanyiwa mwandishi wa habari, au Mbunge.

  5.Kinachotusikitisha zaidi ni maneno ya baadhi ya watu wanaodai kuwa tumepewa pesa ili tuitengeze hii, siyo sawa.

  6.Ukweli ni kwamba tukio ni la kweli na tumepigwa sana, hadi sasa hatuko sawa kiafya.

  7.Siku hiyo, walikuja watu wakiwa na silaha, na wamefunika nyuso zao, wakatuamrisha kuingia ndani ya gari.

  8.Walitufunga macho na kutupeleka kusikojulikana, walitutesa sana, wametupiga sana.

  9.Baada ya kupitia katika kipindi cha mateso makali, tuliachiwa usiku, tukaana kutembea bila kujua tuko wapi.

  10.Siwezi kujua kama tukio hili linahusiana na muziki wangu, maana kuna hadi house boy wetu pia amehusika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *