Mama mzazi wa Wema  Sepetu, Mariam Sepetu amejikuta na wakati mgumu baada ya kupandwa na presha wakati alipokwenda katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar (Sentro) kwa ajili ya kumuona mwanae.

Mama mzazi huyo wa Wema alikwenda kumuangalia mwanawe ambaye anashikiliwa na jeshi la polisi pamoja na wasanii wenzake kwa tuhuma za kuhusika na mtandao wa matumizi na biashara haramu ya madawa ya kulevya.

Mama Wema aliishiwa nguvu na kusaidiwa na ndugu wawili waliokuwa wameambatana naye kituoni hapo na kutolewa nje ya lango kuu la kituo hicho kisha baadae akaoneka kuondoka eneo hilo.

Wema Sepetu anatarajia kupandishwa mahakamani kwa tuhuma za kukutwa na bangi katika nyumba anayoishi.

Muigizaji huyo na wasanii wenzake wa Bongo movie na Bongo Fleva wanashikiliwa na polisi kituo kikuu baada ya kuhusishwa na tuhuma za dawa za kulevya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *