Mbunge wa viti maalum (CCM), Mama Salma Kikwete amelipongeza Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na kampuni ya uchapishaji Longhon ya nchini Kenya kwa kazi kubwa ya kutunga Kamusi Kuu ya Kiswahili.

Mama Salma ambaye ni balozi wa Kiswahili amelishukuru baraza hilo kwa kwa kukuza lugha ya kiswahili ndani ya Afrika na nje ya Afrika.

Akizungumza katika uzinduzi wa Kamusi Kuu ya Kiswahili jijini Nairobi Nchini Kenya, Mama Salma ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema kuwa ithibati hiyo iwe ni ushahidi wa kukubalika kwa Kamusi hiyo kwa matumizi rasmi katika nchi hizo mbili.

Mama Salma amesema kuwa “Kama Balozi wa Kiswahili kwenye Bara letu la Afrika ni kazi kubwa sana ya kutunga kamusi ya Kiswahili na kuiwezesha kupata itifaki ya taasisi zinayosimamia kiswahili katika nchi zote mbili yaani Tanzania na Kenya,”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *