Mama mzazi wa mtoto Zahara aliyeasiliwa na Angelina atamani kumuona mwanae

0
343

Mama mzazi wa mtoto Zahara aliyechukuliwa na kulelewa na muigizaji nyota wa Marekani, Angelina Jolie amesema anataka kumuona na kuongea na mtoto wake baada ya miaka 12.

Angelina Jolie aliamua kumchukua na kumasili mtoto huyo kutokana na mama yake kutokuwa na uwezo wa kumlea na kushindwa kumtibu baada ya kuwa na utapiamlo uliotokana na umasikini wa familia yake.

Mentewab Dawit Lebiso: Mama mzazi wa mtoto Zahara aliyeasiliwa na Angelina Jolie.
Mentewab Dawit Lebiso: Mama mzazi wa mtoto Zahara aliyeasiliwa na Angelina Jolie.

Mtoto huyo alichukuliwa akiwa na umri wa miezi sita ambapo sasa amefikisha umri wa miaka 12 akiishi maisha ya kitajili chini ya muigizaji huyo nyota wa Marekani Angelina Jolie.

Mama mzazi wa mtoto huyo Mentewab Dawit Lebiso wa Ethiopia amesema anataka kumuona mtoto wake na kuongea nae lakini hatomchukua kutokana na Angelina Jolie kufanya kazi kubwa ya kumlea.

Mentewab Dawit Lebiso amesema angefurahi sana kama Angelina Jolie angemruhusu kuonana na mtoto wake na amueleze kuhusu kama yeye ndiyo mama yake mzazi na asili yake ni Ethiopia.

LEAVE A REPLY