Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli leo ameadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa katika Taasisi ya Magonjwa ya Saratani ya Ocean jijini Dar es salaam.

Mama Magufuli amesema ameamua kuwatembelea na kuwafariji wagonjwa hospitalini hapo kwa kutoa msaada huo kwa kuwa yeye alizaliwa katika hospitali hiyo tarehe na mwezi kama wa leo.

Mama Magufuli alipata fursa ya kuwaombea afya njema wagonjwa wote na kuwatia moyo ndugu wanaouguza kuendelea na jukumu hilo zito.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk. Julius Mwaisalage amemshukuru s Mama Janeth Magufuli kwa moyo wake wa kujitolea kwa kusaidia wagonjwa hospitalini hapo kwa kuwa kitendo hicho kinawatia moyo wao kama wauguzi lakini pia kinarudisha imani kwa wagonjwa na kujiona kuwa hawapo peke yao.

Mama Janeth Magufuli kwa kushirikiana na wanawake wa Wilaya ya Ilala na Temeke wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema wametoa msaada wa vitu mbalimbali kama vile mchele, maharage, sabuni za kufulia, sabuni za kuogea, maziwa ya unga,juisi, taulo za kike, vitenge, kanga, misuli,mafuta ya kujipaka na dawa za meno.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *