Muigizaji mkongwe wa Bongo Movie, Grace Mapunda maarufu ‘Mama Kawele’ amewataka wanawake nchini kuacha kubweteka na kutegemea wanaume kwani kufanya hivyo ni sawa na kuukaribisha umasikini mwenyewe.
Mama Kawele aamesema miaka kadhaa iliyopita na sasa hivi ni tofauti, mwanamke wa sasa anatakiwa asiangalie upande mmoja bali asimame kama nguzo katika familia na kuhakikisha anautokomeza umasikini wa kujitakia.
Pia muigizaji huyo amewahimiza wanawake kufanya kazi kwa bidii ili wazikomboe familia zao na kuacha kutegemea wanaume kwa kila kitu kwani maisha sasa yanahitaji kupambana kwa kila mtu ili kuutokomeza umasikini.
Muigizaji huyo aliendelea kwa kusema kuwa wanawake wanaobweteka bila kujishughulisha na kuukubali umasikini kiukweli wananiumiza sana kichwa na apendezwi na tabia hiyo kutokana na mabadiliko yaliopo sasa.
Mwisho aliwataka wanawake wabadili mtazamo wa maisha na wanatakiwa kujitambua zaidi ili kufikia malengo yao waliyojiwekea na siyo kubweta kwa kuwa wanaume wapo.
Picha kwa hisani ya GM