Mama mzazi wa aliyekuwa muigizaji wa Bongo movie, Steven Kanumba aitwae Florence Mutegoa amezindua shindano la kusaka vipaji vya uigizaji “Kanumba Star Search” kwa ajili ya kuigiza filamu itakayoelezea maisha ya marehemu Kanumba.

Uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Idara ya habari maelezo jijini Dar es Salaam ambapo mama Kanumba ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kudhamini shindano hilo litakaloibua vipaji vipya vya uigizaji nchini.

Mama Kanumba amesema kwamba shindano hilo limeandaliwa na kampuni ya Kanumba The Great wakishirikia na AM Arts Promotion hadi sasa inamdhamini mmoja ambaye ni kampuni ya simu ya mkononi KZG-Tanzania.

Vile vile mkurugenzi wa kampuni ya AM Arts Promotion, James Mwombeki amesema kwamba marehemu Kanumba alikuwa na mchango mkubwa sana katika kuitangaza nchi kimataifa pamoja na kuinua vipaji vya wasanii nchi kwa hiyo lazima tumuenzi kupitia sanaa hiyo.

Kwa upande mwingine staa wa bongo movie, Mayasa Mrisho “Maya” amewataka wananchi kushiriki kwa wingi katika shindano hilo kwani sanaa ya uigizaji ni njia moja wapo ya kujipatia kipato.

Shindano hilo linatarajiwa kuanza mwezi septemba kwa mikoa ya kanda ya ziwa baadae mikoa mengine.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *