Baada ya Zari kumtolea maneno machafu Hamisa Mobeto kupitia mitandao ya kijamii, mama mzazi wa Mobeto amemjia juu Zari na kumwambia aachane na mwanae.

Hayo yamekuja baada ya Zari kumtuhumu Hamisa Mobeto kujichora ‘tatuu’ ya mpenzi wake Diamond Platnumz.

Mama mzazi wa Mobeto ameshindwa kujizuia na kujikuta akimtolea maneno Zari juu ya mwanaye huyo.

Zairi akiwa na Diamond
Zairi akiwa na Diamond

Mama Mobeto amesema kuwa hakuna wakati mgumu kama kuona mtoto wake huyo anazungumziwa vibaya kila wakati katika mitandao ambapo wakati mwingine siyo jambo la kweli zaidi ya kumchafua tu.

Jamani mimi kama mzazi, sidhani kama kuna mzazi yeyote anayeweza kuvumilia kuona mwanaye kila mara yuko kwenye midomo ya watu au kuongelewa vibaya kwenye mitandao ya kijamii kwa vitu ambavyo hajafanya,”.

Amesema kuwa habari ambayo imesambaa kuhusu mwanaye kujichora tatuu ya Diamond, anaona ni mambo ambayo hayana msingi wowote zaidi ya kumchafua na kumdhalilisha mwanaye.

Zari alimtolea matusi Mobeto kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii akimtahadharisha juu ya habari zilizozagaa kuwa, huwa anachepuka na Diamond kwa siri hasa mwanamama huyo anapokuwa nyumbani kwake, Afrika Kusini na kumwacha baba watoto wake huyo jijini Dar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *