Mkazi wa Mbande Mbagala jijini Dar es Salaam, Asma Juma ambaye ni mzazi anayedai kujifungua watoto mapacha na kudai kuibiwa mtoto mmoja katika hospitali ya Temeke aeleza kilichotokea.

Asma Juma anawatuhumu wauguzi wa hospitali hiyo kumuiba mtoto wake huyo akidai, awali wakati alipokuwa na ujauzito picha za Ultrasound alizowahi kupima zilionyesha kuwa ana ujauzito wa mapacha.

Alipokuwa hospitalini hapo alimsikia nesi aliyekuwa akimuhudumia akithibitisha kua ana watoto wawili.

Asma amesema, “Wakati nipo chumba cha upasuaji, baada ya kuambiwa nafanyiwa operesheni, yule nesi aliyekuwa ananihudumia akiwa na mtu mwingine nilimsikia akisema ‘viko viwili’ akimaanisha wako watoto wawili, yule nesi aliniambia nisijitingishe, baadaye walinichoma sindano nikapoteza fahamu.”

Pia ameongeza “Nilivyozinduka nikajikuta nipo chumba cha pili nikiwa nasikia maumivu makali sana, niliwaomba dawa wakaniambia nitazikuta wodini hapo hakuna dawa za maumivu.

Baada ya hapo nimeletewa mtoto mmoja saa kumi na moja alfajiri nakumbuka wakati nipo wodini nilimsikia yule nesi aliyekuwa akinihudumia akisema ‘Ultrasound’ zinadanganya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *