Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amechaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoani Kagera (KRFA) baada ya kupata kura 21 kati ya 22.

Uchaguzi huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Optima, Bananzi, wilayani Misenyi mkoani huomo.

Malinzi amekuwa Mwenyekiti wa KRFA toka Machi 17 mwaka 2012 na katika kipindi chake cha kuwa madarakani amesaidia kwa kiasi kikubwa kurejesha hamasa ya soka mkoani Kagera.

Pia Malinzi amesaidia ukarabati wa Uwanja wa Kaitaba ambaao sasa una mwonekano mzuri ukiwa unapambwa na nyasi bandia na utatumika katika michezo ya ligi kuu nchini.

Kwa upande mwingine, Salum Chama amefanikiwa kutetea nafasi yake ya Katibu Mkuu KRFA kwenye uchaguzi huo kwa kupata kura zote 22, wakati Pelegrinius Rutahyugwa alitetea Ujumbe Mkutano Mkuu waTFF kwa kupata kura zote 22.

Huku Didas Zimbihile alitetea nafasi ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu Klabu wa TFF kwa kukusanya kura zote 22.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *