Timu ya taifa ya vijana ya Mali chini ya umri wa miaka 17 imetetea ubingwa wake wa baada ya kuifunga timu ya taifa ya Ghana goli 1-0.

Katika mechi hiyo bao pekee la Mali limefungwa na Momadou Samake na kuihakikishia Mali kutetea ubingwa huo.

Kwa upande wake kocha wa Ghana, Paa Kwesi Fabin amesema kuwa alipanga kikosi chake cha kwanza ambacho kiliifunga Niger 6-5 katika hatua ya penalti kwenye hatua ya nusu fainali.

Kocha huyo ameongeza kuwa pamoja na kupoteza mchezo huo, wachezaji wake walifanya jitihada za kutosha ila bahati haikuwa upande wake.

Mashindano hayo yalifanyika nchini Gabon na Mali kuibuka mshindi pamoja na kuiwakilisha Afrika kwenye mashindano ya kombe la dunia kwa umri huo nchini India mwaka huu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *