Timu za vijana za Ghana na Mali zimefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika chini ya umri wa miaka 17.

Ghana wametinga fainali baada ya kupata ushindi wa penati 6-5 dhidi ya Niger baada ya kwenda sare katika dakika tisini za mchezo.

Mali wao wamefanikiwa kutinga fainali yao ya pili mfululizo baada ya kuwaondosha Guinea kwa penati 2-0 huku kipa wa Mali, Youssouf Koita, akiwa shujaa wa timu hiyo kwa kuokoa michomo mingi na penati

Mchezo wa fainali ya michuano hiyo ya vijana utapigwa jumapili ya tarehe 28 mchezo ukichezwa katika dimba la Amitié Sino-Gabonaise, mjini Libreville,

Mchezo wa kusaka mshindi wa tatu kati ya Niger na Guinea nao utafanyika siku hiyo hiyo ya jumapili katika uwanja wa Amitié Sino-Gabonaise.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *