Waziri mkuu wa Malaysia, Najib Razak amesema kuwa itasafirisha mwili wa ndugu wakiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong – nam kwenda nchini humo kwa maziko.

Waziri mkuu huyo amesema kuwa serikali ilikuwa imeidhinisha kusalamishwa mwili wa Kim Jong-nam nchini kwao.

Bwana kim aliuawa kwenye uwanja wa ndege Kuala Lumpur na kemikali kali mwezi uliopita wakati alipokuwa safarini.

Mauaji hayo yaliasababisha mzozo wa kidiplomasia kati ya Malaysia na Korea Kaskazini.

Waziri mkuu Najib amesema kuwa raia 9 wa Malaysia ambao wamekuwa wakizuiwa kuondoka Korea Kaskazini, sasa wamepewa ruhusa wa kuondoka nayo Malaysia itawaruhusu raia wa Korea Kaskazizi kuondoka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *