Mwanamuziki wa Bongo fleva, Malaika Exervery ‘Malaika’ amesema kwamba katika vitu ambavyo aviwezi kutoweka kichwani kwake ni baada ya kutapeliwa nchini China katika jiji la Hong Kong nchini humo.

Staa huyo amesema kwamba tukio hilo limetokea mara tu baada ya kuwasili nchini humo na kuwekwa kuzuizini kwenye uwanja wa ndege kwa masaa 16 akihisiwa amebeba dawa za kulevya ambapo si kweli.

malaik-452x678

Malaika amesema alinyang’anywa mizigo yake yote hadi simu yake ya mkononi huku akikaa eneo hilo kwa muda mrefu mpaka kuja kuachiwa usiku na kufanikiwa kurudishiwa simu tu lakini mizigo yote walichumchukulia.

Msanii huyo ameongeza kwa kusema kuwa aliporudishiwa simu yake alikuwa anataka kununua laini ya nchini humo ili afanye mawasiliano ndiyo akauziwa laini kwa bei kubwa kuliko kawaida.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *