Staa wa Bongo fleva, Diana Exavery ‘Malaika’ amesema kwamba anachukulia poa video yake kuzuiliwa kutoka na aliyekuwa mpenzi wake, Edward Baruti ‘Eddie’ baada ya wawili hao kutokuwa na maelewano kwasasa.

Malaika amesema kwamaba hapo awali alichanganyikiwa kufuatia kitendo hicho cha mpenzi wake huyo kushikilia msimamo wake kuwa hawezi kuruhusu video ya msanii huyo ya wimbo wa “Raruararua” itoke lakini sasa anachukulia poa tu.

malaikaEddie alifikia uamuzi huo hivi karibuni baada ya kuzinguana na Malaika hivyo kumzuia dairekta aliyetengeneza video hiyo, Hanscana kutoitoa mpaka pale atakapoamua yeye kwani ndiye aliyegharamia kila kitu kwenye video hiyo mpaka ilipokamilika.

Malaika aliongeza kwa kusema kwamba mwanzoni kitendo hiko kilimuuma lakini sasa hivi anachukulia poa tu akiamini mambo yatamnyookea vizuri na huenda video ya wimbo wake huo ukatoka na kuwafikia mashabiki wake.

Mwanamuziki huyo amesema video hiyo ilikuwa bomba sana na alitamani mashabiki wake waione lakini mpaka sasa haijatoka ila anaamini mambo yatakwenda sawa ivi karibini.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *