Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Malaika amefunguka na kusema kuwa watu wanapokuwa wakitumia picha zake au wakiandika mambo yanayohusu maisha yake binafsi ni kitu ambacho kinamuumiza sana.

Malaika amedai kuwa muda mwingine huwa anaudhika na kukasirika pindi anapoona watu wanachangia kwenye mitandao ya kijamii na kuhusisha mambo yake ya kimuziki pamoja na mambo yake ya kifamilia.

Mwanamuziki huyo amesema anapokuwa anapost picha kwenye mitandao ya kijamii wakati mwingine anapata ‘Comments’ mbalimbali nyingine zinakuwa zinaudhi mpaka kupelekea kuumia nafsi yake.

Malaika ameongeza kwa kusema kama mtu ana jambo lolote anataka kumwambia amwambie yeye lakini siyo kuingiza na masuala ya familia yake.

Mwanamuziki huyo kwasasa anatamba na wimbo wake ‘Rarua’ unaoendelea kufanya vizuri katika vituo mbali mbali vya radio na runinga nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *