Washiriki wa Shindano la Dance100% wanaendelea na mafunzo chini ya uongozi wa majaji wa shindano hilo ambapo kila jaji anafundisha makundi mawili kuelekea fainali ya shindano hilo.

Mratibu wa shindano hilo Bhoke Egna amesema majaji wanaendelea kutoa mafunzo ya ushiriki wa faianali kwa kuwatembelea kwenye vituo vyao vya mazoezi.

Bhoke amesema “Kila kundi linaendelea na mazoezi katika eneo lake ambapo majaji wetu wanaendelea kuwafundisha kwa kuwatembelea kwenye maeneo yao ili waweze kuona walivyojiandaa na kuwashauri mambo ya kufanya ili kuweza kufanya vizuri zaidi’ Amesema Bhoke.

Makundi 6 ambayo yalifuzu hatua ya fainali yapo chini ya majaji kama ifuatavyo.

Jaji Super Nyamwela

  1. J Combat Crew
  2. Clevers Boys

Jaji Khalila

1.Team Makorokocho

  1. D.D.I Crew

Jaji Lotus

  1. Wazawa Crew
  2. B.B.K Crew

Fainali ya michuano hiyo itafanyika Septema 24 mwaka huu jijini Dar es Salaam

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *