Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa ataanza kuwastaafisha watumishi wa umma wasiowajibika huku akidai katika ofisi yake ni wakuu wa idara wanne pekee ndio wanaofanya kazi vizuri kati ya watumishi 120.

 

Aidha amesema kuwa daima haogopi kutumbuliwa jipu kama wengi wanavyo muombea na kwamba yuko tayari kugombana na mtu yoyote kwa kutetea wananchi.

Amesema tayari amewasiliana na ngazi za juu za serikali, ili kuona uwezekano wa kuwapunguza watumishi hao ikiwa ni pamoja na kuwastaafisha kwa manufaa ya umma.

Amesema kuna watendaji ambao hawana ubunifu na wengi wamekuwa wakijitetea kuwa hawana bajeti au hawajapata bajeti hizo bila kubuni njia za kutatua changamoto za wananchi.

Akizungumza na watumishi wa halmshauri hiyo, madiwani, wenyeviti wa serikali za mitaa na wabunge wilayani Temeke, leo, Makonda alisema, hayuko tayari kumvumilia mtendaji yoyote ambaye hawajibiki ipasavyo katika kutatua kero za wananchi.

Akiwasilisha ripoti ya wilaya, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva, alisema wamejipanga kikamilifu hususan katika kukabiliana na kero za wananchi, kusimamia ukusanyaji wa mapato, kumaliza changamoto ya madawati ambapo hivi sasa wana wanashughulikia changamoto ya vyumba vya madarasa na uhalifu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *