Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewatangazia walimu wa mkoa wa Dar es Salaam kuanza kusafiri bure kwenye treni baada ya kuingia makubaliano na Shirika la Reli Tanzania (TRL).

Hatua hiyo imekuja ikiwa miezi michache imepita tangu, kiongozi huyo kuanzisha mfumo wa walimu kusafiri bure kwenye daladala wakati akiwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

treni

Makonda amesema walimu watasaifiri bure katika njia za Stesheni ya Ubungo Maziwa na Stesheni ya Pugu ambako treni zinafanya safari zake.

Mkuu wa mkoa huyo amesema kinachotakiwa ni kuwa na vitambulisho kutoka kwa wakuu wa shule, wakionyesha hakuna atakayewahoji hivyo watasafiri bure.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa amesema walimu watasafirishwa kwa nidhamu kubwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *