Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mashindano ya kuibua na kukuza vipaji, Airtel Rising Stars Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi naye atakuwepo kwenye hafla hiyo ambapo Katika uzinduzi huo mchezo wa kwanza utazikutanisha timu za Ilala Boys dhidi ya Bombom.

Dar es salaam inawakilishwa na mikoa yote mitatu kisoka ambayo ni Ilala, Kinondoni na Temeke kwa pande zote mbili za wavulana na wasichana.

Mikoa mengine itakayoshiriki mashindano hayo ni Mbeya, Mwanza na Morogoro kwa upande wa wavulana, Arusha, Lindi na Zanzibar kwa upande wa wasichana.

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *