Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa atavunja nyumba zinazotumika kufanyia biashara ya ngono maarufu kama uwanja wa fisi zilizopo Manzese na badala yake atajenga viwanda vidogo vidogo.

Makonda ameyasema hayo wakati alipotembelea maeneo hayo katika muendelezo wa ziara yake katika jiji la Dar es Salaam kwa lengo la kusikilizwa kero zinazowakabili wananchi wa mkoa huo.

Pia mkuu wa mkoa huyo amesema kuwa nyumba zote za uwanja wa fisi zitabomolewa japokuwa wananchi wanaoishi maeneo hayo huishi maisha magumu.

Makonda leo anamaliza ziara yake ya siku kumi katika jiji la Dar es Salaam ambapo ameseilikiza na kutatua baadhi ya kero zinazowakabili wakazi wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *