Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewatangazia walemavu wenye mahitaji ya miguu katika mkoa wa Dar es salaam kujitokeza siku ya Agosti 14 na 15 kujiandikisha na kupimwa ili waweze kupatiwa miguu ya bandia itakayo wasaidia katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Makonda amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam, amesema siku hiyo kutakuwa na wataalamu (Madaktari) watakao chukua vipimo iliwawatengenezee miguu kulingana na mahitaji.

Makonda ameamua kuwasaidia wananchi wasio na uwezo wa kumudu gharama za vifaa hivyo, ambapo atawapatia miguu hiyo bure, kutokana na wananchi wengi waishio mkoa wa Dar es salaam kutokua na uwezo wa kumudu gharama za manunuzi ya miguu ya bandia pindi wanapopata ajari na kukatika miguu hali

Miguu hiyo yenye thamani ya Shilingi Milion 800 itatolewa bila malipo kwa wananchi waliopata ajali na kushimdwa kupata miguu hiyo kutokana na kushindwa kumudu gharama za kununua miguu hiyo ambapo mguu mmoja unagharimu Milion tatu.

Kwa mantiki hiyo amewatangazia wananchi wote wenye mahitaji ya miguu ya bandia na hawana uwezo wa kumudu gharama kufika ofisini ya mkuu wa mkoa siku ya Jumatatu na Jumanne kwaajili kukutana na wataalamu wa miguu watakaochukua vipimo kwaajili ya kutengenezewa miguu kulingana na maumbile yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *