Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kesho anatarajia kukutana na kufanya mazunguzo na wafanyabiashara wadogo wadogo ili kujua sababu ya kutokuwa tayari kwenda katika maeneo waliyopangiwa.

Makonda alisema lengo la kukutana na wafanyabiashara hao ni kujua kwa nini hawapo tayari kwenda katika maeneo waliyotengewa na kuangalia namna bora ya wao kufanya biashara zao ili kuondoa usumbufu uliopo sasa.

Pia Makonda amesema hawezi kuruhusu utaratibu unaofanywa na machinga hao, ambao baada ya kauli ya rais wamerejea na kuweka biashara zao hata sehemu za watembea kwa miguu na kusababisha kero.

Wafanyabiashara wadogo wadogo (wamachinga) wamekuwa wakifanya biashara maeneo ya watembea kwa miguu baada ya kauli ya Rais Magufuli ya kuwaruhusu wafanyabiashara hao waachwe kufanya biashara katika miji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *